27 Novemba 2025 - 21:17
Vyombo vya Habari vya Israel: Kuongezeka kwa Nguvu ya Iran na Muungano wa Muqawama “Kunatia Wasiwasi”

Maafisa wa Idara ya ujasusi ya Israel walisema kuwa endapo mzozo mpya baina ya Iran na Israel utazuka, basi kisasi cha Iran kitaifanya Israel ikabiliwe na hatari kubwa zaidi kuliko ile iliyoshuhudiwa katika tukio lililopita.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Gazeti la Jerusalem Post la Israel limeandika kuwa kuna wasiwasi mkubwa nchini Israel kufuatia kuongezeka upya kwa nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na washirika wake baada ya vita vilivyodumu kwa siku 12.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maafisa wa Idara ya Ujasusi ya Israel waliiambia hivi karibuni Kamati ya Masuala ya Kigeni na Ulinzi ya Knesset kwamba Hezbollah inaendelea kujihami upya kwa kasi kubwa kuliko uwezo wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) wa kuharibu maghala yake kwa mashambulizi ya angani.

Vyombo vya Habari vya Israel: Kuongezeka kwa Nguvu ya Iran na Muungano wa Muqawama “Kunatia Wasiwasi”

Walisema kuwa endapo mzozo mpya baina ya Iran na Israel utazuka, basi kisasi cha Iran kitaifanya Israel ikabiliwe na hatari kubwa zaidi kuliko ile iliyoshuhudiwa katika tukio lililopita.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha